• Home
  • About Us
  • Schools
    • Thaqalayn Nursery School
    • Dar-ul-Muslimeen Primary School
    • Al-Qaem Seminary
    • Islamic College
  • Welfare
    • Safiina Dispensary
    • Holy Ramadhan Charity
  • Contact
  • Blog
Registration

Thaqalayn Nursery School

start your Child's Career with us today!
'FOMU ZA MAOMBI' ya nafasi za masomo kwa Mwaka 2022 zitapatikana Shuleni, KUANZIA TAREHE 01/10/2021, kwa TShs. 20,000/- . Wahi, nafasi ni chache. KARIBUNI.
Enrol with us Today

MAELEKEZO MUHIMU KUHUSU THAQALAYN NURSERY SCHOOL

  • Thaqalayn Nursery ni shule pamoja na madrassa ya kiislam ya watoto itumiayo lugha ya kiingireza katika kujifunza na kufundisha.
  • Nafasi za Masomo zipo wazi kwa watoto wenye umri kati ya miaka 3 ½ - 4 ½. Nafasi hutolewa kwa anayewahi kabla hazijaisha, hakuna ubaguzi wa rangi, kabila, lugha, wala dini.
  • Muhtasari (syllabus) ni wa miaka mitatu.
  • Watoto watawekwa katika madarasa kulingana na umri wa kila mtoto.
  • Muhtasari wetu unaendana na ule wa kimataifa wa kiwango cha “Montessori” ambapo kila mtoto hupata uangalizi, huduma na upendo wa karibu sana. Pia kila mtoto hufundishwa kwa kadri ya kiwango cha uelewa wake.
  • Masomo ya msingi ya Quran na mafunzo ya elimu ya dini ya kiislamu hufundishwa.
  • Masomo yote hufundishwa kwa mbinu na ujuzi wa hali ya juu kuhusisha matumizi ya saikolojia, zana na vifaa bora vya kufudindishia kwa kuzingatia umri mchanga wa watoto.
  • Shule yetu huwaandaa watoto vema na kuwapa msingi imara na muhimu katika kuwawezesha watoto kupata nafasi katika shule za umma, shule za kimataifa na zile shule zitumiazo lugha ya kiingereza hapa nchini na nje ya nchi.
  • Mwaka wa Masomo huanzia Mwezi Januari kila mwaka na kuishia mwezi Desemba. Mwaka hugawanywa katika mihula miwili ambapo mtoto hupata likizo ndogo na kubwa katika mwaka.
  • Masomo yafundishwayo ni: Konsonanti na Irabu za Kiingereza na Kiswahili, Kiingereza cha kuzungumza na kusoma, Hisabati na kuhesabu namba, Elimu ya Mazingira, sanaa na ufundi, Quran Elimu ya dini ya Kislam, Michezo na nyimbo.
  • Pia shule huwapa watoto uji wakati wa kipindi cha mapumziko.
  • Kila muhula, shule itatoa majaribio na mitihani ili kupima na kutathimini, maendeleo ya mtoto kitaaluma na wazazi watapewa matokeo ya majaribio hayo.
  • Kila mwaka, shule itatoa mitihani ya mwisho wa mwaka ambapo watoto watapanda madarasa kulingana na ufaulu wao.
  • Baada ya kuhitimu masomo ya muda ya miaka miwili katika shule yetu ya Nursery mtoto atapewa cheti cha kuhitimu na pia ataruhusiwa kuendelea na masomo ya Pre-Primary katika shule ya Msingi Dar-ul-Muslimeen kama ataweza kufikia viwango katika interview ya Pre-Primary.
  • Upo usafiri wa basi ambapo huduma hutolewa katika maeneo yanayofikika kwa sasa.
Copyright © 2021. All Rights Reserved for the 'Registered Trustees of Dar-ul-Muslimeen'.
Contacts
+255 26 2323086 muslimbhanji@gmail.com
muslim
Address
Plot 17/2 CBP, Veta Road, Near CBE Makole, DODOMA City TANZANIA
Follow Us

We use cookies to enable essential functionality on our website, and analyze website traffic. By clicking Accept you consent to our use of cookies. Read about how we use cookies.

Your Cookie Settings

We use cookies to enable essential functionality on our website, and analyze website traffic. Read about how we use cookies.

Cookie Categories

Essential

These cookies are strictly necessary to provide you with services available through our websites. You cannot refuse these cookies without impacting how our websites function. You can block or delete them by changing your browser settings, as described under the heading "Managing cookies" in the Privacy and Cookies Policy.

Analytics

These cookies collect information that is used in aggregate form to help us understand how our websites are being used or how effective our marketing campaigns are.