Madrasat Ahlulbayt Islamic College
MAELEKEZO MUHIMU KUHUSU MADRASSAT AHLULBAYT
- Lengo la Madrassah hii ni kuandaa vijana wasomi kwa mafunzo ya dini ya Kiislamu na kuwahamasisha vijana kwa njia ya dini.
- Kozi itakayotolewa katika Madraza hii itakuwa: “CHETI KATIKA MAARIFA YA KIISLAM”.
- Kozi na ya miaka minne (4).
- Masomo yatakayo fundishwa yatakuwa pamoja na: Tajweed Al-Quran, Tafseer Al-Quran, Tadabbur Al-Quran, Hadithi, Taarikh al-Islam, Fiqhi, Usul Al-Fiqhi, Mantiq, Falsafa, Usluub Al-Khitaabah, Usluub Al-Tabligh, Lugha Al-Arabiyyah, Nahw, Sarf, Adyaan Al-Muqaarinah, Akhlaq Al-Islami, Aqaid Al-Islami, n.k.
- Baada ya kufaulu na kumaliza kozi kwa miaka minne, cheti kitatolewa na kupangiwa kazi ya kulingania dini (tabligh).
- Waombaji baada ya mafanikio pia wanaweza wakakabidhiwa shughuli kama vile ualimu au wahubiri katika sehemu wanaotoka ili wafanikishe shughuli za kidini.
- Ingawa Madrassah hii inatoa Elimu bure na kinawapa wanafunzi mahitaji yanayostahili, kama malazi, chakula, n.k., hii isiwe sababu kwa wazazi wa wanafunzi kujikalia tu bila kutoa mchango wao wa kihali na mali wakati wa dharura.
- Mapendekezo yamepewa wale ambao umri wao ni kati ya miaka 14 hadi 22 (wavulana tu), na walio umri wa ziada wanaweza kufikiriwa kutokana na kiwango cha elimu walio nao.