Thaqalayn Nursery School
start your Child's Career with us today!
MAELEKEZO MUHIMU KUHUSU THAQALAYN NURSERY SCHOOL
- Thaqalayn Nursery ni shule pamoja na madrassa ya kiislam ya watoto itumiayo lugha ya kiingireza katika kujifunza na kufundisha.
- Nafasi za Masomo zipo wazi kwa watoto wenye umri kati ya miaka 3 ½ - 4 ½. Nafasi hutolewa kwa anayewahi kabla hazijaisha, hakuna ubaguzi wa rangi, kabila, lugha, wala dini.
- Muhtasari (syllabus) ni wa miaka mitatu.
- Watoto watawekwa katika madarasa kulingana na umri wa kila mtoto.
- Muhtasari wetu unaendana na ule wa kimataifa wa kiwango cha “Montessori” ambapo kila mtoto hupata uangalizi, huduma na upendo wa karibu sana. Pia kila mtoto hufundishwa kwa kadri ya kiwango cha uelewa wake.
- Masomo ya msingi ya Quran na mafunzo ya elimu ya dini ya kiislamu hufundishwa.
- Masomo yote hufundishwa kwa mbinu na ujuzi wa hali ya juu kuhusisha matumizi ya saikolojia, zana na vifaa bora vya kufudindishia kwa kuzingatia umri mchanga wa watoto.
- Shule yetu huwaandaa watoto vema na kuwapa msingi imara na muhimu katika kuwawezesha watoto kupata nafasi katika shule za umma, shule za kimataifa na zile shule zitumiazo lugha ya kiingereza hapa nchini na nje ya nchi.
- Mwaka wa Masomo huanzia Mwezi Januari kila mwaka na kuishia mwezi Desemba. Mwaka hugawanywa katika mihula miwili ambapo mtoto hupata likizo ndogo na kubwa katika mwaka.
- Masomo yafundishwayo ni: Konsonanti na Irabu za Kiingereza na Kiswahili, Kiingereza cha kuzungumza na kusoma, Hisabati na kuhesabu namba, Elimu ya Mazingira, sanaa na ufundi, Quran Elimu ya dini ya Kislam, Michezo na nyimbo.
- Pia shule huwapa watoto uji wakati wa kipindi cha mapumziko.
- Kila muhula, shule itatoa majaribio na mitihani ili kupima na kutathimini, maendeleo ya mtoto kitaaluma na wazazi watapewa matokeo ya majaribio hayo.
- Kila mwaka, shule itatoa mitihani ya mwisho wa mwaka ambapo watoto watapanda madarasa kulingana na ufaulu wao.
- Baada ya kuhitimu masomo ya muda ya miaka miwili katika shule yetu ya Nursery mtoto atapewa cheti cha kuhitimu na pia ataruhusiwa kuendelea na masomo ya Pre-Primary katika shule ya Msingi Dar-ul-Muslimeen kama ataweza kufikia viwango katika interview ya Pre-Primary.
- Upo usafiri wa basi ambapo huduma hutolewa katika maeneo yanayofikika kwa sasa.