Dar-ul-Muslimeen Primary School
Tangazo
Maelekezo Muhimu Kuhusu Dar-ul-Muslimeen Primary School
- Dar-ul-Musliomeen Primary School hutumia kiingereza kama lugha ya kufundishia na kujifunzia.
- Shule inaendeshwa na wadhamini waliosajiliwa wa Dar-ul-Muslimeen hapa Tanzania kama taasisi inayosaidia na kuhudumia jamii.
- Shule inatoa elimu ya msingi kwa muda wa miaka saba yaani kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la saba kwa kufuata mtaala na muhtasari wa Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya elimu iliyochini ya Wizara ya Elimu.
- Masomo yafundishwayo hapa shuleni ni Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Sayansi na technologia, Jiografia, Historia, Uraia, Stadi za kazi kama yalivyoelekezwa na mtaala na muhtasari wa masomo Tanzania.
- Baada ya miaka saba ya masomo, wanafunzi hufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi darasa la saba ambao huandaliwa na Baraza la mtihani la Taifa Tanzania.
- Wanafunzi hufundishwa pia masomo ya Quran, Maarifa ya dini ya kiislamu na pia somo la Adabu na Tabia njema.
- Tabia na mwenendo mwema ni kigezo muhimu na cha lazima katika kumfanya mtoto kuendelea na masomo shuleni hapa.
- Kila darasa huwa na idadi ya wanafunzi kati ya 40 – 45 tu. Wanafunzi ambao huchelewa kutimiza masharti ya kujiunga huingizwa katika orodha ya kusubiri.
- Mwaka wa Masomo huanzia Mwezi Januari na kuishia mwezi Disemba kila mwaka. Kuna mihula miwili ya masomo ambayo huwa na wiki za masomo kati ya 22. Pia kila muhula hufuatiwa na likizo ya takribani mwezi mmoja. Hivyo kuna mihula miwili na likizo tatu kwa mwaka. Maelezo zaidi yapo katika kalenda ya shule.
- Kila mwaka wanafunzi watafanya mitihani minne ili kupima na kutathimini maendeleo yao kitaaluma. Matokeo ya mitihani hiyo hupewa wazazi. Viwango vya kufaulu kwa madarasa ya awali mpaka darasa la pili ni wastani wa alama 70% na kuanzia darasa la tatu mpaka la sita ni wastani wa alama 60%.
- Watoto wote wanaoombewa nafasi hapa shuleni hupaswa kufanya mtihani wa udahili na wale wanofaulu tu ndio huandikishwa na kupatiwa nafasi.